Thursday, July 1, 2010

UBELGIJI WACHUKUA URAIS WA UMOJA WA ULAYA

Ubelgiji imechukua rasmi Uwenyekiti wa Umoja wa Ulaya kutoka kwa Uhispania.

Haya yanatokea licha ya nchi hiyo kuwa chini ya utawala wa serikali ya muda ikisubiri kundwa serikali mpya. Inaendelea kuongozwa na waziri mkuu, Yves Leterme tangu serikali yake ya muungano ilipoanguka mwezi Aprili.

Hii itakuwa mara ya kumi na tatu kwa Ubelgiji kushikilia wadhifa huo unaozunguka kati ya nchi wanachama kila baada ya miezi sita.

Hivi sasa majukumu ya wadhifa huo hata hivyo yamepungua kutokana na mkataba wa Lisbon ambao ulianza kufanya kazi mwishoni mwa mwaka jana.

Malengo ya Ubelgiji kwa miezi sita ijayo ni pamoja na kuundwa chombo kipya cha kusimamia shughuli za fedha na mkataba juu ya ushirikiano imara zaidi wa kiuchumi miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.
.

No comments:

Post a Comment