Sunday, July 4, 2010

WATU 220 WAUAWA NCHINI CONGO

Kiasi ya watu 220 wameuwawa na idadi kama hiyo wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa likisafirisha mafuta kupinduka na kulipuka mashariki ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Mripuko huo ulisababisha nyumba moja kushika moto ambako watu walikuwa wakiangalia mechi ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia. Baadhi ya watu waliuawa walipojaribu kuchota mafuta kutoka lori hilo.

Sababu ya ajali au mripuko uliofuatia, haijulikani. Helikopta za Umoja wa Mataifa zilisaidia kuwasafirisha majeruhi hospitali. Wanajeshi wa Congo ambao walipoteza baadhi ya wenzao, pia walisaidia katika kazi za uokozi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wanajeshi watano kutoka vikosi vyake vya amani,waliuawa walipokuwa wakijaribu kuwazuwia watu kukaribia lori hilo.

No comments:

Post a Comment