Tuesday, July 20, 2010

MAMBO YA BIG BROTHERS ALL STARS


Yale maisha ya siku 91 ndani ya jumba huko Afrika Kusini yajuilikanayo kwa jina la Big Brother All Stars yameanza rasmin siku ya jumapili ambapo washiriki wapatao 14 kutoka katika nchi hizo hizo 14 wameingia katika jumba hilo.

Kwa mara nyengine tena Tanzania imepata nafasi ya kuingiza mwakilishi wake ndani ya jumba hilo ambe kwake yeye hii itakua ni mara ya pili kushuriki shindano hilo nae ni Mwisho Mwampamba, ambapo kwa mara ya kwanza yalipoanzishwa mashindano hayo miaka 7 iliyopita alishiriki.

Lakini kwa upande wake Mwisho inaonekana kama hakuanza vyema maisha ya nyumbani humo kwani jana Jumatatu alipoitwa kwenye diary room Big Brother alimtaka ataje majina mawili ya watu ambao angependa kuwaning'iniza kwa ajili ya kutolewa ndani ya jumba hilo lakini mwisho alishindwa kutaja hata jina moja kwa kile alichodai kwamba hakua akijua jina la mshiriki hata mmoja aliyeko ndani ya jumba hilo.

Kutokana na sheria za nyumbani humo kitendo hicho cha Mwisho kutomtaja mtu yoyote kimepelekea yeye mwenyewe kujitundika na kusubiri kupigiwa kura na matokeo kutangazwa siku ya Jumapili, na kama akipata kura za kumtosheleza anaweza kubakia na kuendelea na maisha ya humo ndani, lakini kama hakupata kura za kutosha, siku ya Jumapili itakua ndio mwisho wa maisha ya humo ndani kwa mwakilishi huyo pekee kutoka Tanzania.

No comments:

Post a Comment