Mwili wa Makamu wa Rais wa chama cha upinzani kisichosajiliwa nchini Rwanda cha Green Party Andre Kagwa Rwisereka, umekutwa karibu na gari lake wiki moja baada ya kutoweka kwake.
Polisi pamoja na chama hicho wamesema kuwa mwili wa kiongozi huyo ulikutwa kwenye eneo lenye maji karibu na mto Mukula kusini mwa mji wa Butare.
Msemaji wa polisi Eric Kayiranga amesema watu waliyomuona usiku kabla ya kutoweka wamesema alikuwa na fedha nyingi kwahivyo wanahisi huenda lilikuwa ni tukio la ujambazi.
Mwanzilishi wa chama hicho cha Democratic Green Party Frank Habineza amesema Rwisereka ulichinjwa,ingawaje kichwa kilibaki na mwili.
Chama cha Democratic Green kimeshindwa kupata usajili utakaokiwezesha kushiriki katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi ujayo.
Makundi yanayotetea haki za binaadamu yameilaumu serikali ya Rwanda kwa kukandamiza upinzani pamoja na vyombo vya habari kuelekea kwenye uchaguzi huo
No comments:
Post a Comment