Saturday, July 3, 2010

AHMADA UMELEWA - LUGHA TATA? KIMEFICHIKA NINI?

Mtu mmoja ananitumia ujumbe kuniuliza, ' e vipi mbona wimbo huu nasikia umepigwa marufuku Visiwani?'
Nami namwuliza, "kulikoni hata wimbo wenyewe siufahamu?"

Ananifahamisha jina la wimbo, 'Ahmada Umelewa'
Nauliza, "ama, sababu hasa ya kufungiwa?"

Naye anigeuza kauli, 'mbona swali ndilo hilo nililokuuliza?'
Nami namjibu, "basi ukaona nakujibu swali kwa kuuliza swali, jua kuwa jibu lake sinalo. Na heri niwaulize wengine."

Ati, lugha iliyotumika katika wimbo huu imefichika?

Baada ya kuusikiliza wimbo, wala sioni kilichojificha zaidi ya pale anaposema '...amekaa na fungu la watoto na mikono mfukoni, mmoja kamtoa shilingi, kamrusha ukutani...' hapo nakiri asilani sijaelewa sentenso hiyo. Basi, kuondoa hilo, mie naona Ahmada anaaswa kuacha unywaji pombe, ujeuri na kutukana wazee.

Ama? kweli hiyo? ati, "Ahmada Umelewa" imekatazwa kusikika redioni huko Visiwani? Ah. Yawezekana ni uzushi tu.

***Wavuti

No comments:

Post a Comment