Jumla ya wahamiaji haramu 21 wamekamatwa baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria na Idara ya uhamiaji Zanzibar kwa kushirikiana na Kikosi cha Kuzuwia Magendo KMKM katika Maeneo ya Tumbatu Unguja.
Katika taarifa yake Afisa Uhusiano wa Idara hiyo Muhsin Abdalla Muhsin amekiri kukamatwa kwa watu hao wakiwa ni raia wa Kenya ,Somali na Ethiopia ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.
Amesema wamepata taarifa ya kukamatwa kwa watu hao siku ya Jumamosi na kikosi cha KMKM kwa msaada wa wananchi kutoa taarifa ya uwepo kwa watu hao .
Hata hivyo watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa zaidi ambapo wanagundua kuwepo kwa wageni ambao wanawatilia mashaka ili hatua za kiusalama ziweze kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment