Thursday, June 17, 2010

WABUNGE 3 WAACHIWA KWA DHAMANA KENYA

Wabunge wawili nchini Kenya na Waziri mmoja msaidizi waliokuwa wameshtakiwa kwa uchochezi nchini humo wameachiliwa kwa dhamana.

Waziri msaidizi wa barabara Wilfred Machage na Mbunge wa Mlima Elgon Fred Kaondi waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mmoja, ilhali mbunge mwenzao wa Cherangany Joshua Kutuny akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili pesa taslimu.

Mwanaharakati mwingine aliyeshtakiwa pamoja na wabunge hao, Christine Nyagitha pia aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja. Wote wanne walifikishwa leo asubuhi mbele ya Jaji wa Mahakama kuu, na walikanusha mashtaka dhidi yao.

Mahakama hiyo pia iliwaagiza wanasiasa hao wawe wanafika katika afisi za idara ya upelelezi, CID kila siku asubuhi saa tatu. Wabunge hao walishtakiwa kwa makosa ya kutoa vitisho vya kuwatimua watu kutoka katika ardhi zao, iwapo mswada wa katiba mpya utapitishwa. Kesi yao itasikizwa tena Juni 21 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment