Sunday, June 13, 2010

MASHAMBULIO YA MAGURUNETI MJINI BUJUMBURA

Watu sabaa wamejeruhiwa, maguruneti yaliporipuliwa jana usiku mjini Bujumbura na vituo kadhaa vya chama tawala kutiwa moto mikoani.
Msemaji wa polisi Pierre Chanel Ntarabaganyi anasema mashambulio hayo "yamelengwa kuuwa na yameandaliwa wakati mmoja".
Ni kitendo cha kutaka kufuja uchaguzi wa rais-amesisitiza msemaji huyo wa polisi.Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa vikosi vya usalama,ambae hakutaka jina lake litajwe anautuhumu upande wa upinzani kuwa nyuma ya mashambulio hayo.
Msemaji wa Muungano wa kidemokrasi kwa ajili ya demokrasia,LĂ©onard Nyangoma amesema upande wa upinzani hauhusiki hata kidogo na mashambulio hayo.Visa hivi vinatokea katika wakati ambapo hali ni tete nchini Burundi.
Upande wa upinzani unakosoa matokeo ya uchaguzi wa May 24 uliokipatia ushindi mkubwa chama tawala cha CDNN-FDD.Kampeni za uchaguzi wa rais zimeanza rasmi jana.Na uchaguzi utaitishwa June 28 mwaka huu.
.

No comments:

Post a Comment