Tuesday, June 1, 2010

MARUFUKU KWENDA KOMBE LA DUNIA: GHANA

Rais wa Ghana amewapiga marufuku mawaziri wake pamoja na maafisa wengine wa serikali kwenda Afrika kusini kuangalia fainali za kombe la dunia hadi pale watakapokuwa na majukumu ya kiserikali katika fainali hizo.

John Martey Newman, msemaji wa rais John Atta Mills , amesema kuwa amri hiyo ina lengo la kuhakikisha kuwa shughuli za kiserikali hazivurugiki wakati wa fainali hizo, ambazo zinaanza rasmi barani Afrika kwa mara ya kwanza Juni 11.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ghana , Black Stars, moja kati ya matumaini makubwa ya bara hilo , ilikuwa ni timu ya kwanza kufanikiwa kupata tikiti ya kushiriki fainali hizo za kombe la dunia mwaka 2010, na itakumbana na Ujerumani, Serbia na Australia katika kundi D.

No comments:

Post a Comment