Israel imewauwa wapiganaji watano wa Kipalestina katika ukanda wa Gaza leo, watatu katika mashambulio ya anga baada ya shambulizi la roketi dhidi ya ardhi ya Israel na wawili wengine katika mapambano mengine ya ardhini.
Jeshi la Israel limethibitisha kuwa ndege zake zimeshambulia wapiganaji katika ukanda wa Gaza na kwamba watu wawili wenye silaha wameuwawa baada ya kuvunja amri ya kutokaribia uzio wa mpaka katika eneo la pwani, lakini haikutoa taarifa zaidi.
Msemaji wa kundi la Popular Resistance Committees amesema kuwa wanachama watatu wa kundi hilo wameuwawa katika shambulio la Israel katika eneo la kaskazini mwa Gaza, mmoja akiwa kamanda wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment