Sunday, May 9, 2010

VIONGOZI WA ULAYA WAILINDA EURO


Viongozi kadhaa wa Ulaya wamefuta mipango ya kuhudhuria kumbukumbu ya kumalizika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia barani Ulaya zinazofanyika leo na badala yake wanaziimarisha jitihada za kuilinda sarafu ya Euro.


Marais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy na Italia Silvio Berlusconi hawatahudhuria kumbukumbu hiyo inayofanyika mjini Moscow, Urusi.

Hata hivyo, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel tayari amewasili Moscow kwa ajili ya kuhudhuria kumbukumbu hiyo. Wakati huo huo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajaribu kutayarisha mkakati ya kuilinda sarafu ya Euro kabla masoko ya fedha duniani hayajafunguliwa tena kwa biashara hapo kesho.

Matatizo ya kiuchumi ya Ugiriki yanayoendelea yameiweka sarafu ya Euro katika hatari, licha ya mataifa mengine yanayotumia sarafu hiyo kuahidi kuisaidia Ugiriki kiuchumi. Kwa upande wake Kansela Merkel ana matumaini kuwa msaada mpya kwa Ugiriki utasaidia kuondoa wasi wasi katika masoko ya fedha.


Mkutano wa dharura utakaowakutanisha mawaziri wa fedha wa nchi zote 27 za Umoja wa Ulaya umepangwa kufanyika hii leo.


.

No comments:

Post a Comment