Sunday, May 9, 2010

WINGU LA MAJIVU KUATHIRI USAFIRI WA NDEGE ULAYA

Mripuko mwingine unaosababisha wingu la majivu katika mlima wa volkano nchini Iceland ni kitisho tena kwa usafiri wa ndege na utaendelea kuathiri usafiri wa ndege katika maeneo mengine barani Ulaya.

Maafisa wa ndege nchini Italia wamefunga anga ya usafiri kaskazini mwa nchi hiyo leo kutokana na mkusanyiko wa wingu la majivu. Hapo jana Uhaspania ilifunga viwanja 19 ukiwemo uwanja wa kimataifa ulioko mjini Barcelona.

Shirika linaloshughulikia usafiri wa ndege barani Ulaya linatabiri kwamba kutakuwa na msururu wa wingi la majivu leo utakaoathiri anga kutoka Greenland hadi Ireland na pia visiwa vya Azores na Madeira katika bahari ya Atlantic.

No comments:

Post a Comment