Saturday, May 8, 2010

VIONGOZI WA ENEO LA EURO WALINDA UTHABITI WA THAMANI YA SARAFU HIO

Viongozi wa mataifa wanachama wa sarafu ya euro wamezindua mipango ya kuunda mfuko mpya wa dharura wa kulinda sarafu yao ya euro. Katika mkutano uliofanyika jana usiku mjini Brussels, viongozi hao 16 wamekiri kuwa mzozo wa madeni ya Ugiriki, umelitosa eneo hilo katika hali ya dharura.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, amesema kuwa mfuko huo mpya utatoa ishara ya wazi na kwamba wana nia ya kuweka ulinzi imara wa sarafu ya euro wakati masoko yatakapofunguliwa hapo Jumatatu. Nae rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa anaunga mkono juhudi za viongozi hao wa Ulaya.

Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya, watafanya mkutano mwingine wa dharura kesho Jumapili, kutunga mpango wa kupambana na biashara ya kubahatisha katika masoko ya hisa dhidi ya sarafu ya euro. Wabunge wa bunge la Ujerumani, jana ijumaa, waliidhinisha kwa thuluthi-mbili ya kura mpango wa kuiokoa Ugiriki .

Ujerumani , itaipatia Ugiriki kiasi cha euro bilioni 22 kwa mujibu wa mpango huo.

.

No comments:

Post a Comment