Saturday, May 1, 2010

TAKRIBAN WATU 28 WAMEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA MABOMU SOMALIA

Miripuko miwili ya bomu iliyotokea ndani ya msikiti imeua hadi watu 28 katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Kwa mujibu wa maafisa, watu wengine 70 wamejeruhiwa.

Miripuko hiyo ilitokea pale watu walipokuwa wakingojea sala ya adhuhuri ndani ya msikiti.

Inasemekana kuwa wanamgambo wa Al-Shabab husali katika msikiti huo wa Abdalla Shidiye, ulio karibu na soko la Bakara.

Kwa mujibu wa Redio Shabelle nchini humo, kiongozi mmoja wa Al-Shabaab alijeruhiwa katika shambulio hilo wakati alipokuwa akihubiri.

Mapigano yamepamba moto upya mjini Mogadishu majuma ya hivi karibuni. Raia wengi waliuawa katika mapigano yaliyozuka kati ya wanajeshi na waasi katika eneo hilo hilo, siku chache zilizopita.

.

No comments:

Post a Comment