Jana hapa Uholanzi ilikua ndio ziku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Malkia hapa Beatrix na sherehe hizi kwa kawaida hufanyika kila siku ya mwisho ya mwezi wa nne, na watu huazimisha siku hii kwa kufanya sherehe mbali mbali, lakini jambo ambalo hufanywa katika kila pembe ya Uholanzi ni lile la kuuza vitu kwa bei ya chini kabisa mitaani na shemu nyengine hupanga vitu barabarani na kuuza, na mimi nilipata kutembelea Centre ya mji wetu na hali ilikua kama ifuatavyo
Hapa kulikua na baskeli nyingi za kufanyia mazoezi na kila anaetaka ilikua anaingia na kufanya mazoezi ya pamoja kwa kufata maelekezo ya walimu wanaoendesha mazoezi hayo.
Na hawa ndio walimu waliokua wakiendesha mazoezi hayo ya baskeli ambapo ilionekana shughuli hii ilidhaminiwa na Rabobank
Huyu aliyejitia rangi alikua akigawa mabofu kwa watoto wanaopita karibu yake.
Watu walikua n wengi ambapo kila mmoja ilikua hukosi kumuona na mfuko ikiashiria kwamba keshapata cha kununua.
Kulikua pia na sehemu ya kufurahishia watoto.
Wafanya biashara wakiwa wametandika na kumwaga bidhaa zao chini tayari kwa kuuza
.
No comments:
Post a Comment