Saturday, May 8, 2010

MTANZANIA KAPEWA MIAKA 14 NA KURUDISHWA TANZANIA

Mtanzania wa kabila la Kisukuma mwenye umri wa miaka 36 ambaye tarehe 26 Oktober 2009 aliua mkewe Bi Anne Holmstrom umri wa miaka 27 wa Denmark ambaye walikutana Tanzania na kuoana mwaka 2003.

Katika mauaji hayo yasemekana alitumia njia ya kumnyonga mke wake kwa waya za umeme na baadaye kutumia "machate/mapanga" kwa kuukata kata mwili wake vipande vipande, amepata hukumu ya miaka 14 kuwepo jela na atakapomaliza kifungo chake atarudishwa Tanzania moja kwa moja kutokea jela.

Kufuatana na habari zilizotolewa mtanzania huyo alihamaki baada ya mke kuomba waachane kufuatana na kitendo cha mume kujihusisha na mwanamke mwingine akiwa likizo Tanzania.

Kitu ambacho
Scandinavien ni makosa makubwa hata kusababishwa watu kupeana talaka za kuachana, wanakuwa na mtazamo wa ndoa ni za milele kifo ndiyo huwatenganisha na kama mtu hajapata makaratasi ya kudumu ya kuishi nchini kufuatana na sheria huwepo katika mipangilio ya kurudishwa nchini kwake.

Huyu mtanzania ilikuwa arudishwe siku ya pili yake mara tuu baada ya kuachana na mkewe, haya yalimchanganya kichwani na kufanya uamuzi wa mauaji kwa mkewe watoto zake wakiwa wapo shule ya vidigi-digi

.

No comments:

Post a Comment