Saturday, May 8, 2010

MARUFUKU DHIDI YA TIMU YA TOGO YAONDOLEWA

Timu ya taifa ya Togo, iliyokuwa imepigwa marufuku kushiriki katika Kombe la mabingwa barani Afrika, sasa itaruhusiwa kushirki katika michuano hiyo, baada ya Rais wa shirikisho la kandanda duniani Sepp Blatter kufikia makubaliano na Shirikisho la soka Afrika CAF mjini Zurich.

Timu ya Togo ilijiondoa katika mashindano ya Kombe la Afrika yaliyofanyika mapema mwaka huu nchini Angola, baada ya watu wawili wa ujumbe wao, pamoja na dereva wa basi lao kuuawa wakati timu hiyo iliposhambuliwa katika eneo la Cabinda.

Wakati ulimwengu mzima ulikuwa umeshtushwa na kusikitishwa na shambulio hilo, Togo ilipigwa marufuku kwa miaka minne, kwa sababu ya kujitoa katika mashindano bila ya kufuata taratibu.

.

No comments:

Post a Comment