Saturday, May 1, 2010

MAFUTA YAZIDI KUSAMBAA KATIKA GHUBA YA MEXICO



Mafuta yanayovuja kutoka katika kisima kwenye eneo la ghuba ya Mexico yameanza kuenea hadi ufukweni katika jimbo la Louisiana jana na hivyo kuwa kitisho cha janga la kimazingira.

Rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina wa janga hilo.

Siku ya Alhamisi upepo mkali kutoka kusini mashariki ulisukuma utando wa mafuta hayo hadi katika mwambao ulioko katika eneo ambalo mto Mississipi huingia baharini.

Shirika la mafuta la Uingereza , BP limesema litawajibika vilivyo kutokana na kuvuja kwa mafuta hayo na litalipa fidia kwa madai yatakayotolewa kuhusiana na janga hilo.

Kwa mujibu wa wataalamu, makadirio ya mwanzo ya kusafisha utando huo wa mafuta yatagharimu kati ya Dola bilioni mbili na bilioni tatu.

.

No comments:

Post a Comment