Monday, May 10, 2010

HONGERA!!!!!!!!!!!


Assalaamm alaikum.
Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kukubaliana na matokeo ambayo yametokea kwa mwaka huu katika nynja ya soka, kwa sababu katika watu wengi wanaoshindana ni lazima mmoja wao aibuke mshindi, kwa mantiki hii nachukua fursa hii kuwapa hongera wapenzi na washabiki wote wa Chelsea kwa jitihada iliyochukuliwa na timu yao hadi kufikia kutwaa ubingwa kwa mwaka huu wa 2009/10.
Nawapa hongera maalum rafiki zangu wakiwemo Dula Rasta ambae tulikua pamoja katika kufuatilia mechi hizi kwa njia ya TV kwa msimu mzima, Farid wa Leuven, Bwasa akiwa maeneo ya Liege.
Mwisho ningewapa pole wale washabiki wenzangu wa timu nyengine zote zilizobaki ambazo zimebahatika kushika nafasi kuanzia ya pili na kuendelea, ila napenda kuwasihi msije mkachukua uamuzi kama aliouchukua yule shabiki wa Arsenal kule Kenya, kwa sababu hii ni burudani tu na si jengine.
.

No comments:

Post a Comment