Friday, May 7, 2010

HAKUNA CHAMA KILICHOPATA WINGI MKUBWA KABISA WA VITI KATIKA UCHAGUZI WA UINGEREZA

Zoezi la kupiga kura limemalizika katika uchaguzi wa nchini Uingereza na hesabu zilizopatikana hadi sasa zinaonyesha kuwa nchi hiyo inaelekea kwenye mabadiliko ya serikali.

Chama cha kihafidhina kinachoongozwa na David Cameron kimepata viti vingi lakini hakikufanikiwa kupata wingi mkubwa kabisa.

Chama cha leba cha waziri mkuu wa hadi sasa Gordon Brown kimepungukiwa viti bungeni.

Hata hivyo bwana Brown amechaguliwa tena katika eneo lake la Scotland.

Katika hotuba ya shukurani kwa kuchaguliwa tena katika eneo lake bwana Brown ameashiria kuwa huenda bado akaendelea kuwa na sauti katika kuundwa kwa serikali mpya.

Kati ya vyama vya Conservative na Leba, kimesimama chama cha Liberal Democrats kinachoweza kuwa mwamuzi juu ya kuundwa serikali mpya japo chama hicho kipo nyuma katika idadi ya vipi.

.

No comments:

Post a Comment