Tuesday, April 6, 2010

ZANZIBA KUADHIMISHA SIKU YA AFYA DUNIANI LEO NA KESHO KUWAOMBEA DUA MZEE KARUME NA NYERERE

Zanzibar imeamua kuadhimisha Siku ya Afya Duniani leo badala ya kesho ili kuepusha sherehe za siku hii kuingiliana na siku ya kumkumbuka Rais wa mwanzo wa Zanzibar Mzee Abeid Karume ambae aliuawa tarehe 7 April 1972.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh, Sultan Mohammed Mukheiry alisema jana alipofanya mazungumzo na vyombo vya habari kwamba Zanzibar itaadhimisha Siku ya Afya Duniani leo, kwa sababu kesho kutakua na Dua pamoja na mambo mengine katika kumkumbuka aliyekua Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Karume pamoja na aliyekua Rais wa Tanganyika Julius Nyerere pamoja na viongozi wengine ambao walipigania uhuru wa nchi.

Katika kumkumbuka Mzee Karume, Watanzania wanatarajiwa kujumuika pamoja na kusoma Dua ambayo imetajwa kufanyika Zanzibar huku Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mh, Jakaya Kikwete ndie atakaekua mgeni rasmin katika Dua hio.

Kwa mujibu wa radio ya Sauti ya Tanzani Zanziba Mh, Kikwete anatarajiwa kuwasili Zanzibar mchana wa leo na anatarajiwa kupokea matembezi ya hiari ambayo yalianzia Makunduchi Ijumaa iliopita, matembezi ambayo yalipangwa na Chama Cha Mapinduzi kwa kutambua uongozi wa Marume ambapo viongozi kadhaa kutoka vyama vya upinzani kikiwemo kile cha CUF wanatarajiwa kushiriki katika mapokezi ya matembezi hayo pamoja na Dua ambayo itasomwa kesho.

.

No comments:

Post a Comment