Tuesday, April 6, 2010

HATUA ZA VIZA YA SCHENGEN ZABADILIKA

Umoja wa Ulaya umezindua mfumo wa pamoja wa utoaji visa kwa mataifa yaliyoko katika makubaliano ya Schengen, ambao unawaruhusu wageni kuingia katika eneo la mataifa ya Schengen , eneo la mataifa ya umoja wa Ulaya ambapo mipaka iko wazi kati ya mataifa jirani.

Licha ya kuwa mataifa yote yaliyoko katika makubaliano ya Schengen yanaweza kutoa visa kwa eneo hilo, hadi hivi sasa kila nchi ilikuwa na utaratibu wake.

Hivi sasa mfumo huo utakuwa unaratibiwa, na kwa mujibu wa halmashauri ya Ulaya utakuwa wazi zaidi na wa hakika. Mfumo huo mpya unaweka muda wa mwisho wa wiki mbili kwa muombaji kuhojiwa katika ubalozi na maafisa wataamua iwapo watoe visa katika muda wa siku 15.

Ni lazima itolewe sababu iwapo viza itakataliwa na kwa mara ya kwanza kwa wale wanaokataliwa watakuwa na haki ya kudai haki kisheria katika nchi zote 25 wanachama wa Schengen

.

No comments:

Post a Comment