Wednesday, April 28, 2010

WAZIRI WA KWANZA WA KIISLAM NCHINI UJERUMANI AAPISHWA


Waziri wa kwanza wa Kiislamu nchini Ujerumani ameapishwa kuwa waziri wa masuala ya jamii katika serikali ya jimbo la Lower Saxony.

Mwanasheria Aygül Özkan mwenye asili ya Kituruki, aliteuliwa kwa kauli moja na chama cha Christian Demokratik CDU na cha kiliberali FDP katika jimbo hilo.

Siku chache zilizopita Özkan mwenye umri wa miaka 38, alizusha hasira aliposema kuwa misalaba haipaswi kuwepo katika shule za serikali. Jumatatu alibadili kauli hiyo.

Mbali na Özkan, wanachama wengine watatu wa CDU vile vile wameapishwa kushika nyadhifa za waziri katika jimbo hilo.

Tangu ulipopatikana muungano wa Ujerumani miaka ishirini iliyopita, kwa mara ya kwanza ameteuliwa Mjerumani kutoka mashariki kuwa waziri katika serikali ya jimbo la magharibi.

Bibi Johanna Wanka ataiongoza wizara ya sayansi katikaserikali ya jimbo la Lower Saxony.

.

No comments:

Post a Comment