Wednesday, April 28, 2010

RAIA 14 WAUAWA KATIKA MAPAMBANO YALIYOZUKA MOGADISHU SOMALIA

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, hadi raia 14 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa nchini Somalia katika mapambano yaliyozuka kufuatia shambulio la kujitolea muhanga lililofanywa na waasi katika mji mkuu Mogadishu.

Watu 4 walijeruhiwa katika shambulio hilo,nje ya kambi ya vikosi vya Umoja wa Afrika. Miongoni mwa majeruhi hao ni wanajeshi 2 wa Umoja wa Afrika.

Vikosi vya usalama kutoka Uganda na Burundi vinaisaidia serikali ya Somalia na vinalinda vituo muhimu kama vile uwanja wa ndege na bandari.

Tangu mwanzoni mwa mwaka 2007, waasi wanapigana dhidi ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na nchi za magharibi.

Sasa makundi ya waasi hao yanadhibiti sehemu kubwa ya maeneo ya kusini na katikati ya Somalia, wakati serikali ikiwa katika eneo dogo la mji mkuu.

Hadi raia 21,000 wameuawa tangu uasi huo ulipoanza nchini Somalia.


.

No comments:

Post a Comment