Monday, April 12, 2010

WATU 11 WAUAWA KATIKA AJALI YA TRENI ITALY

Kiasi watu 11 wameuwawa katika ajali ya treni kaskazini mwa Italia.

Shirika la habari la Italia, Ansa, linaripoti kuwa kiasi cha watu 20 pia wamejeruhiwa, baadhi vibaya sana.

Treni hiyo iliacha njia baada ya kugonga sehemu yalipotokea maporomoko ya ardhi mapema leo asubuhi karibu na mji wa Merano.



.

No comments:

Post a Comment