Wednesday, April 28, 2010

Ushahidi wa Vitambulisho vya wakaazi hewa wa Zanzibar

Kitambulisho cha Msumbiji upande wa mbele
Kitambulisho cha Msumbiji upande wa nyuma
Kitambulisho cha Zanzibar upande wa mbele
Kitambulisho cha Zamznibar upande wa nyuma


Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuwa Wazanzibari wanaostahiki kupewa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi ZAN ID wananyimwa na badala yake wasiofaa kama vile wazaliwa na waakazi wa Tanzania Bara na hata nje ya Tanzania wanapewa.

Wazanzibari hutakiwa kuwa na Cheti cha Kuzaliwa, kupitia kwa Sheha mpaka apate kitambulisho cha Mzanzibari, lakini wageni wanabebwa na kujua njia za kufanya na kupata vitambulisho ambavyo hatimae vinawewezesha kuwa wapiga kura na kuingia katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura DKWK.

Uchunguzi umefanikiwa kupata raia wa Msumbiji akiwa na kitambulisho cha upigaji kura cha nchi ya Msumbiji ikimaanisha kuwa ama ni raia wa nchi hiyo au ni mpira kura, lakini pia akiwa na kitambulisho cha Mzanzibari ambacho kitamuwezesha pia kuwa mpiga kura hapa Zanzibar.

Kwa sasa Tanzania hairuhusu kuwa na uraia wa nchi mbili.

Ushahidi upo kwenye picha, bonyeza picha na tumia mishalle kunavigate kwenye kulia na kushoto kujionea mwenyewe

Shukurani za dhati ziende kwa:

* Mhe Salim Bimani
* Hassan Abdillah Masoud
* Ally Saleh
* Na wote walioshiriki kufanikisha makala hii


***MZALENDO.NET


.

No comments:

Post a Comment