Tuesday, April 27, 2010

MFALME WA UBELGIJI AKUBALI BARUA YA KUJIUZULU KWA LETERME


Mfalme wa Ubeligiji Albert wa Pili ameipokea barua ya kujiuzulu kwa serikali ya Waziri Mkuu Yves Leterme.

Lakini kwa sasa serikali itaendelea kufanya kazi. Uchaguzi mpya unatazamiwa kufanywa mwanzoni mwa mwezi wa Juni.

Serikali hiyo imeshindwa kumaliza mgogoro unaoendelea kati ya Wabeligiji wanaozungumza Kifaransa na wale wanaotumia lugha ya Kiholanzi, kuhusu njia ya kugawa mikoa ya uchaguzi katika eneo la Brussels.

Hapo awali Mfalme wa Ubeligiji alikataa kupokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa waziri mkuu.

Amesema mzozo huo wa serikali unaweza kuathiri wadhifa wa Ubeligiji katika Umoja wa Ulaya. Nchi hiyo inatazamiwa kushika wadhifa wa urais katika Umoja wa Ulaya tarehe mosi mwezi Julai.

.

No comments:

Post a Comment