Tuesday, April 27, 2010

UGIRIKI YATAKA MSAADA WA UMOJA WA ULAYA NA IMF

Ugiriki inahitaji msaada wa dharura wa fedha, ama sivyo serikali itashindwa kulipa madeni yake

Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Giorgos Papakonstantinou alitamka hayo katika hotuba yake bungeni mjini Athens.

Amesema,deni la Euro bilioni 9 linapaswa kulipwa na serikali ifikapo tarehe 19 mwezi Mei.

Wakati huo huo vyombo vya habari nchini Ugiriki vimeripoti kuwa waziri Papakonstantinou alizungumza kwa simu pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, lakini havikueleza yale yaliyojadiliwa.

Hata hivyo mjini Berlin, Kansela Merkel na waziri wa fedha Wolfgang Schäuble wamesisitiza kuwa uamuzi wa msaada huo utapitishwa baada ya kukamilishwa majadiliano yanayofanywa kati ya Kamisheni ya Ulaya, Shirika la Fedha la Kimataifa- IMF na serikali ya Ugiriki.

Mpango unaojadiliwa unahusika na mikopo ya dharura ya hadi Euro bilioni 45.Umoja wa Ulaya unatazamiwa kutoa Euro bilioni 30 huku Ujerumani pekee ikichangiaa Euro bilioni 8.4. Na Euro bilioni 15 zingine zitatoka kwa IMF.


.

No comments:

Post a Comment