Monday, April 26, 2010
BASHIR ACHAGULIWA RAIS SUDAN
Omar Hassan al-Bashir ametangazwa kuwa mshindi wa urais nchini Sudan katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi uliofanyika nchini humo mwanzoni mwa mwezi huu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo, Abel Alier ametangaza matokeo leo na kuongeza kuwa al-Bashir ameshinda kwa asilimia 68 ya kura.
Katika upande mwingine wa nchi hiyo eneo la Sudan Kusini lenye utawala wa ndani kiongozi wa eneo hilo Salva Kiir ametangazwa rais wa eneo hilo.
Akitangaza ushindi huo, Bwana Alier amesema kuwa Kiir ameshinda kwa kupata asilimia 92.2 ya kura zilizopigwa eneo la kusini mwa Sudan.
Bwana Kiir pia atachukua nafasi ya makamu wa kwanza wa rais wa Sudan katika serikali ya muungano wa kitaifa kati ya kaskazini na kusini.
Uchaguzi huo wa Sudan umefanyika kabla ya kura ya maoni upande wa kusini mwezi Januari mwakani juu ya mustakbali wa eneo hilo kama linataka kujitenga au kubakia sehemu ya Sudan.
.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment