Tuesday, April 6, 2010

SPITALI YA HAPA MJINI KWETU ALMELO

Jana jioni nilipita maeneo ya hapa Spitali ya Almelo na nikaona nikuleteeni na nyinyi muone jinsi mazingira ya hapa yalivyo.

Kwa kweli hapa hata kama ukiingia ndani ya Spitali huwezi ukajua kama uko Spitali tofauti na pale Mnazi Mmoja ambapo kuna harufu maalum ukisikia tu ile harufu basi unajua kama upo Mnazi Mmoja hata kama ukifumbwa macho na baadhi ya wakati unalazimika kuziba pua ili kuepuka uvundo unaonuka pale.

Nakumbuka kuna kipindi TVZ ilionesha wadudu kama mende wakiwa wamezagaa katia Spitali ya Mnazi Mmoja pia na magodoro yakiwa yamechakaa vibaya lakini kwa bahati mbaya badala ya serikali kuchukua hatua kwa wafanya kazi wa Spitali kwa kushindwa kuweka mazingira safi ilibidi mwandishi aliyeripoti habari ile apatiwe uhamisho na akapangiwa kwenda kuzoa majani kwenye kiwanja cha kufurahishia watoto (Kariakoo) licha ya vyeti vyake vya uandishi wa habari alivonavyo eti anaambiwa kaitia aibu Serikali.

Huu mji sio mkubwa lakini hii Spitali ni kubwa na ina kila aina ya huduma tofauti na kwetu ambako hata mtu akivunjika mguu anaambia aende Muhimbili, kwa kweli sijui lini tutafika.


Hii ni sehemu ya mbele ya Spitali
Sehemu ya nyuma ya Spitali ambayo kwa sasa inazidi kufanyiwa matengenezo

Hapa ni ubavuni mwa Spitali ambapo kuna sehemu ya kuegeshea baskeli
Sehemu ya mbele ya Spitali kuna eneo kubwa la kuegesha gari
Na hili lote ni eneo la kuegeshea gari


.

No comments:

Post a Comment