Tuesday, April 6, 2010

MAMBO YA KERMIS



Jana katika pita pita mitaani nilikutana na Kermis ambapo niliona nayo ni vyema nikaiweka ili niwakumbushe pale Kariakoo kwani inafanana sana ila sisi kwetu tulishindwa kuiendeleza ingawa ilikua ikiingiza pesa pamoja na kuburudisha watu siku za Siku kuu, lakini Kermis hizi za wenzetu zinatofautiana kidogo na ile Kariakoo yetu, kwa sababu hizi zao wanaziweka tu sehemu kwa muda wa siku chache na baadae huziondosha na kuelekea sehemu nyengine na ile Kariakoo ilpo tu pale pale haiondoki
Hii ni pembea mfano kama ile pembea ya farasi pale Kariakoo


Hili ni banda la biashara, hapa kuna aina ya mchezo wa bahati nasibu na ukishinda unapewa zawadi ya doll
Hii ni pembea ya viti kama vile vya gari la farasi hua vinazunguka kwa aina ya kupanda mlima na kushuka.
Hili pia nalo ni banda la biashara aina ya bahati nasibu, kuna mipira midogo midogo mitatu unainunua ikisha kunakua na makopo yamepangwa kwenye vyumba vyumba kwa hio kwa kutumia hio mipira mitatu unatakiwa kuyapiga yale makopo na kuyaangusha yote na ukifanikiwa unapewa zawadi ya doll.
Hii ni pembea ya vigari nayo inakwenda kwa namna ya kupanda mlima na kushuka lakini hii inakwenda kwa kasi sanakulinganisha na vile vyenye umbo la gari ya farasi na pia hivi huenda mbele na baadae vinarudi kinyume nyume.
Hivi pia ni vigari lakini hiviunakua unaviendesha wewe mwenyewe na kuzunguka utakavyo kwenye uwaja wake na mara nyingi watu hufanya mchezo wa kugongana gongana
Na hili pia ni banda la biashara ya bahati nasibu
Hili ni pembea la viti ambalo linapanda juu na kushuka chini kwa mtindo wa kuzunguka



Hii ndio Kermis yetu sisi pale Tibirinzi Chake Chake Pemba sasa sijui kama ilikua ikifanya kazi ya kufurahisha watu bure? maana kama ilikua ikifanya kazi kwa pesa isingeshindwa kujihudumia mpaka ikafikia hali hii.

.

1 comment:

  1. Tatizo la nyumbani hakuna kiongozi anemjali mtoto na ndio maana Kariakoo imekua kama msitu wa jozani na hii Tibirinzi utazani iliingia moto, wenzetu kila siku wanaumiza vichwa kutafuta mambo gani yatawanufaisha wananchi wakati viongozi wetu kila siku wanaumiza vichwa ni jinsi gani watawabana wananchi na kujinufaisha wao.

    ReplyDelete