Tuesday, April 6, 2010

JESHI LA UHOLANZI LAFANIKIWA KUIOKOA MELI YA UJERUMANI


Jeshi la wanamaji la Uholanzi limefanikiwa kuikomboa meli ya mizigo ya Ujerumani na mabaharia wake 15, waliyokuwa wametekwa na maharamia wa Kisomali umbali wa kilometa 800 nje ya mwambao wa Somalia.

Wizara ya ulinzi ya Uholanzi imesema wanajeshi wake wamewakamata maharamia 10 ambao waliingia ndani ya meli hiyo jana asubuhi.

Hakuna baharia yoyote kutoka Ujerumani aliyejeruhiwa katika tukio hilo, ingawa mwanajeshi mmoja wa kikosi cha wanamaji kutoka Uholanzi amepata majeraha madogo.

Wakati huo huo, manowari ya kijeshi ya Korea Kusini imefanikiwa kuikomboa meli ya mafuta iliyokuwa imebeba mapipa milioni moja na nusu ya mafuta ghafi yenye thamani ya euro milioni 100. Meli hiyo ilitekwa nyara na maharamia wa Kisomali siku ya Jumapili kiasi kilometa 1,500 kusini-mashariki mwa Ghuba ya Aden.

Meli hiyo ilikuwa na mabaharia 24. Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa halina mipango ya kuingia ndani ya meli hiyo iliyokuwa imetekwa nyara.

.

No comments:

Post a Comment