Watuhumiwa 11 wa uharamia kutoka Somalia , wanaoshtakiwa kwa mashambulio mawili tafauti dhidi ya manowari mbili za Marekani nje ya pwani ya Afrika, wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya mjini Virginia nchini Marekani leo.
Washtakiwa watatakiwa kujibu mashtaka ya uharamia na umilikaji silaha ambapo wanakabiliwa na kifungo cha maisha pindi wakipatikana na hatia.
Watano kati yao walikamatwa mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya manowari ya Kimarekani USS Nicholas kufyatuliana risasi na mashua ilioshukiwa kuwa ya maharamia, magharibi mwa Seychelles, nje ya pwani ya Afrika mashariki.
Wengine sita, walikamatwa walipoanza kuifyatulia risasi manowari ya USS Ashland tarehe 10 mwezi huu iliokuwa imeteremsha nanga kiasi ya kilomiata 600 nje ya mwambao wa Djibouti.
.
No comments:
Post a Comment