Friday, April 30, 2010

UBELGIJI NI NCHI YA MWANZO ULAYA KUPIGA MARUFUKU VAZI LA BURQA

Ubeligiji ni nchi ya kwanza ya Ulaya kupiga marufuku mavazi ya burqa na niqab yanayofunika nyuso.

Siku ya Alkhamisi,
wabunge kwa kauli moja walipitisha sheria inayopiga marufuku mavazi ya Kiislamu yanayoficha kabisa nyuso za wanawake hadharani.

Lakini haijulikani lini sheria hiyo itaanza kufanya kazi. Ubeligiji hivi sasa, inakabiliwa na mgogoro wa ndani wa kisiasa na uchaguzi mpya.

Sheria kama hiyo inajadiliwa pia nchini Ufaransa na Uholanzi huku sauti zikizidi kupazwa nchini Austria,Denmark na Uswisi kutaka sheria kama hiyo.



.

No comments:

Post a Comment