Thursday, April 8, 2010

BINADAMU WAPYA WAGUNDULIKA AFRIKA KUSINI

Mabaki ya viumbe wawili wanaofanana na binadamu jambo ambalo si kawaida (hominids) wamegundulika Afrika Kusini.

Kisukuku cha mwanamke mtu mzima na mtoto wa kiume, ikidhaniwa kuwa ni mama na mtoto wake, wana umri wa chini ya miaka milioni 200 tu.

Walipatikana katika mabaki ya mapango mjini Malapa, eneo ambalo si mbali na mji wa Johannesburg.

Watafiti wameliambia jarida la kisayansi kwamba viumbe hao wanakamilisha pengo lililopo baina ya 'hominid' wenye umri mkubwa zaidi na kundi la viumbe wa kisasa 'Homo'.

Mwanadamu kisayansi huwekwa katika kundi la 'Homo'.Watafiti hao wamewapa viumbe hao wapya jina la kisayansi la Australopithecus sedib.


.

No comments:

Post a Comment