Friday, April 9, 2010

BABU SEYA KUKATA RUFAA TENA

Mwanamuziki mwenye asili ya Congo Babu Seya amepanga kufanya jaribio jengine la kukata Rufaa kwake yeye na mwanawe Papii Kocha baada ya lile la mwanzo ambalo lilifanikiwa kuwaachia huru wanawe wawili na kuwarudisha tena jela yeye na Papii.

Wakili ambae anamtetea Babu Seya katika rufaa yake hio Mabere Marando amesema leo kwamba wanatarajia kuwasilisha maombi ya kuangaliwa upya kwa hukumu katika Mahakama ya Rufaa leo hii.

Hii itakua ni mara ya pili kwa Babu Seya na mtetezi wake Mabere Marando kuwasilisha maombi katika Mahakama hio hio ambayo iliwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya Nguza Mbagu na Francis Nguza na kuwarudisha tena kwenye kifungo cha maisha Babu seya na Papii Kocha.

Kwa upande wake nae Mabere Marando alisema kua wanatarajia kuomuomba Jaji Mkuu kuongeza Mahakimu watakaosikiliza kesi hio na hii ni kutokana na uzito wa kesi yenyewe, au kubadilisha Mahakimu.


.

No comments:

Post a Comment