Monday, April 26, 2010

MIAKA 26 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Leo, tarehe 26 April, Tanzania inaadhimisha miaka 46 tangu kuundwa Muugano wa nchi mbili zilizokuwa huru, Tanganyika na Zanzibar.

Kuzaliwa kwa Tanzania kulijiri katika wakati wa kusisimua wa kumalizika ukoloni katika nchi nyingi za Afrika na kuchomoza hisia za kutaka Umoja wa Bara zima la Afrika, na hata Afrika nzima iwe na serikali moja.

Mmoja kati ya mashahidi wa kuzaliwa Muungano wa Tanzania ni Hassan Nassor Moyo, aliyekuwemo katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mapinduzi yaliofanyika miezi mitatu tu kabla ya kuundwa Muungano huo; na pia akatumikia serikali ya Muungano baadae.

Othman Miraji alizungumza naye na kumuuliza kwanza kile kilichowachochea watu waliouasisi Muungano huo, marehemu marais wa Tanganyika na wa Zanzibar, Julius Nyerere na Abedi Karume, kuja na wazo hilo...


.

No comments:

Post a Comment