Sunday, March 7, 2010

ZFA YASIFU MAFANIKIO YA LIGI


PAMOJA na kuendesha Ligi Kuu ya Zanzibar bila ya waudhamini chama cha soka visiwani humo [ZFA] kimesifu mwenendo wa ligi hiyo tangu ilipoanza mwezi uliopita.

Katibu mkuu wa ZFA, Massoud Attai aliliambia Mwananchi jijini jana kuwa ligi hiyo inaendelea vizuri na timu zote ziko katika hali nzuri na wanategemea kumpata bingwa katika hali nzuri kama walivyotarajia.

Alisema: ''Mashindano yanaendelea vizuri bila wasiwasi ni mafanikio kwa kuwa kila kitu kinaenda kama tulivyotarajia, lakini kama wadhamini watajitokeza itakuwa vizuri na tutawajulisha.''

Ligi hiyo inayoendeshwa kwa mtindo wa mzunguko, leo itaingia mzunguko wa tatu kwa timu za Duma kupambana na Konde kwenye Uwanja wa Gombani wakati JKU itacheza na Mundu Uwanja wa Mao.

Hata hivyo hadi sasa kabla ya matokeo ya jana, Malindi ndiyo inaongoza Ligi kwa pointi sita baada ya kushinda mechi zake zote za mzunguko wa kwanza na wa pili.

No comments:

Post a Comment