Wednesday, March 10, 2010

WIZI WA NYAYA ZA UMEME WAATHIRI URUDISHAJI WA UMEME ZAZIBAR

Licha ya wanchi wengi wa kisiwa cha Unguja kufurahia upatikanaji upya wa huduma ya umeme kisiwani hapo, huduma ambayo ilikosekana kwa muda wa miezo mitatu, lakini wakazi wa baadhi ya mitaa bado wanaendelea kukosa huduma hio kufuatia wizi wa nyaya katika maeneo kadhaa ya mji wa Unguja.

Meneja wa Shirika la umeme Zanzibar Bwana Hassan Mbarouk alisema, tumefurahi kwa kufanikiwa kurudisha umeme kwa sababu tulikua hatulali kutokana na ukosefu wa umeme ambao ni muhimu katika maendeleo ya Taifa letu.

Alisema kwamba Shirika lake limepoteza zaidi ya shilingi bilioni 2 ikiwa ni malipo ya wateja kwa mwezi tangu kukosekana kwa huduma hio hapo Disemba 10 mwaka jana, alisema mafundi wazalendo walishirikiana na mafundi kutoka Uingereza, Afrika Kusini pamoja na Norway kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme kisiwani, lakini hata hivyo kuna uharibifu wa baadhi ya vifaa vya umeme.

Meneja huyo alisema ingawa umeme ulirejesha siku ya Jumatatu lakini kuna nyumba nyingi zitakosa umeme kutokana na wizi uliofanywa wa nyaya za kupitishia umeme ambazi ni za shaba pamoja na mafuta katika baadhi ya transfomer.

"Umeme tayari umeshawashwa lakini kuna baadhi ya maeneo yamekosa umeme kutokana na wahalifu kuiba vifaa", meneja huyo alieleza kua polisi wamewahusisha na wizi huo watu wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu kisiwani Unguja.

Wakati huo huo watu watatno wamefikishwa katika mahakama ya mwera jana kwa madai ya kuhusika na wizi wa mita 550 za waya wa umeme ambao una thamani ya shilingi 1.5m,watuhumia wote walipelekwa rumande baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana.

Waziri wa Maji Ujenzi Nishari na Ardhi Mh Masour Yussuf Himid amesema kua Serikali inataka kuhakikisha kua hakutajitokeza tena kwa tatizo la umeme Zanzibar.

"Tunataka kuzibadilisha nyaya za zamamni zilizochakaa za megawatts 40 ambazo zimepita chini ya bahari kwa kuweka nyengine mpya za megawatts 100 kwa msaada wa USAID"alisema Waziri Mansour.

Alisema pia Serikali inanunua majenereta ya hakiba na pia imepanga kutafuta njia nyengine ya vyanzo vya umeme kama vile jua, upepo na mawimbi ya bahari.

Tatizo hili la umeme Unguja lilianza tarehe 10 Disemba ambapo tatizo kama hilo lilitokea mnamo mwaka 2008, tatizo hilo linatokana na uchakavu wa nyaya zilizopita chini ya bahari ambazo zina miaka 40 sasa tangi zitandikwe.

Hata hivyo wananchi wameonesha furaha yao baada ya kurudi kwa umeme ambao ulikosekana kwa muda mrefu.

"Najisikia furaha sana baada ya kurudi kwa umeme, ilikua ni huzuni kwangu na ninaamini na kwa wenzangu pia, bi Khadija Omar mama mwenye watoto wanne, alielezea kwa furaha.

Abdalla Abbas ambae ni mwanafunzi amesema, kwa bahati mbaya tumekua tukisoma katika mazingira magumu huku tukitumia mishumaa, lakini kwa kutudi umeme, tunapaswa kufurahi

No comments:

Post a Comment