Tuesday, March 2, 2010

WAKENYA NA SAFARI ZA UARABUNI

Kuotokana na ukosefu wa kazi raia wa Afrika Mashariki wamekua wakielekea ng'ambo au pia arabuni kwa tamaa za kupata ajira na pesa nyingi, baadhi yao huangukia modomoni mwa walaghai wanaowapora, au hata kuwatumwa kwa kazi ambazo hawakutarajia, na wengine hata kuishia utumwani.

Mjini Mombasa takriban watu miatatu wameingia katika mtego kama huu ambapo imepelekea kupiga kambi nje ya ofisi moja ya wakala ambae inadaiwa kua ametoweka na mamilioni ya pesa baada ya kuwaahidi kua atawapeleka kufanya kazi Uarabuni.

Wazee na vijana, wasichana na wavulana, wakiwa na hasira wanataka pesa zao, walikua wameahidiwa na bwana Rishad Amana ambae ni mfanya biashara na mwana siasa mashuhuri katika pwani ya kenya, kwamba kuna nafasi za kazi Dubai.

Bwana huyo alitangaza kwenye redio kua kuna kazi huko dubai hivyo anahitaji vijana 280 ambao atawasafirisha na kuwapeleka kwenye kazi huko dubai, watu hatimae wakajitokeza kwenye ofisi zake na kuanza kujiandikisha pamoja kulipa pesa alizokua akizihitaji ambazo inadaiwa mwanzo alisema anataka shilingi 16,000 pesa za Kenya, lakini baade idadi hio ya pesa iliongezeka na kufikia 22,500 pesa za Kenya.

Baada ya kupokea pesa kutoka kwa watu aliowasajili, akawapa ahadi ya kua baada ya wiki mbili watakua wameshasafiri, baada ya wiki mbili kupita kimya kilikua kimetawala kwa watu waliokua wakisubiri safari hio na ndipo walipoamua kufunga safari kwenda kwenye ofisi za bwana huyo, na ndipo walipokuta ofisi hizo zimefungwa na yeye mwenyewe kukosekana.

Lakini jana Jioni bwana Amana amejitokeza lakini kwanza kabisa alijisalimisha kwa baraza la Maimamu na waumini nchini Kenya, nalo baraza la Maimamu likamkutanisha bana Amana na watu wanaodaiwa kua amechukua pesa zao katika ukumbi maarufu sana mjini Mombasa wa Almeida.

Sheikh Mohammed Idris ni mwenyekiti wa baraza la Maimamu alisema "Shuhuli hii ya ndugu yetu Rishad Amana tumeichukulia umuhimu kwa sababu waliotoa pesa ni vijana wetu na yeye ni kijana wetu, kwa hio umeona ni lazima tupange akutane nao pamoja ili awaeleze ukweli ulivyo".

Sasa ikawa zamu ya mfanya biashara Rishad Amana kuzungumza na umati nae alisema, "mimi ni mwana siasa wa pwani na mimi ni mwana siasa wa kitafa, yale yaliyotokea ilinibidi kutokea, ndugu zangu munisamehe sana kila wiki mimi nitalipa watu ishirini kutokea jumamosi, mimi nipate time ya kwenda mbio kutafuta pesa zenu na kuwalipa watu ishirini".

Na baadae ndipo ikawa zau ya watu waliofikwa na kadhia hio nao kutoka maoni yao juu ya usemi huo wote wa bwana Amana, manadada mmoja ambae alionekana kua na hasira alisema"mimi nilimpa in dollas kwa ujinga wangu mwenyewe watu wote walipa in Kenya Money, kwa hivyo sisi hatutaki mambo mengi, pesa kwisha, stori zake na barala la Maimamu atajuana mwenyewe".

Hata hivyo Maimamu walifaulu kuwashawishi umati uliokua umejaa katika ukumbi huo wa Almeida , kumpa mfanya biashara huyo nafasi ya kupumua ili aweze kuwatafutia pesa zao.

No comments:

Post a Comment