Saturday, March 20, 2010

WAISRAELI NA WAPALESTINA WAREJEE KATIKA MAJADILIANO

Majadiliano ya amani kati ya Israel na Wapalestina yaliyokwama, huenda yakaanza upya hivi karibuni. Hiyo ni kwa mujibu wa wapatanishi wa kimataifa waliokutana Moscow nchini Urusi siku ya Ijumaa.

Wajumbe wa Marekani,Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya na Urusi - maarufu kama kundi la pande nne- walikutana kujadili mapendekezo mapya, kwa azma ya kuwarejesha Wapalestina na Waisraeli katika meza ya majadiliano.

Mjumbe maalum katika Mashariki ya Kati, Tony Blair amesema, ni matumaini yake kuwa karibuni utapatikana mpango utakaoanzisha majadiliano yasio ya uso kwa uso. U.N. Secretary General Ban Ki-moon, left, and Russian President Dmitry Medvedev enter a hall for talks in Moscow's Kremlin on Thursday, March 18, 2010.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewahimiza Waisraeli na Wapalestina kutekeleza wajibu wao katika jitahada za kutafuta amani.

Lakini, pendekezo lililotolewa kwa Israel na Wapalestina kuanzisha majadiliano ya amani na kupata suluhisho la mataifa mawili, limepokewa kwa maoni mbali mbali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigdor Liebermann alipozungumza ziarani mjini Brussels alisema, Israel haitokubali kushinikizwa kwa kile alichokiita "kanuni za bandia na kipindi kisichozingatia hali halisi." Wakati huo huo, mpatanishi mkuu wa Wapalestina, Saed Erakat ameuliza vipi itahakikishwa kuwa Israel kweli itasitisha ujenzi wa makaazi ya walowezi.

Wajumbe wa kundi hilo la pande nne wameitaka Israel isitishe moja kwa moja ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo inayoikalia na kurejea katika meza ya majadiliano. Lengo ni kupata mkataba kuhusu taifa la Palestina lililo huru na lenye uwezo wa kuendelea kuwepo. Wamesema, mkataba huo upatikane katika kipindi cha miezi 24 ijayo.


.

No comments:

Post a Comment