Saturday, March 20, 2010

WAHUDUMU WA BRITISH AIRWAYS WAANZA MGOMO WA SIKU TATU


Wahudumu wa shirika la ndege la British Airways wameanza mgomo wa siku tatu baada ya majadiliano ya kujaribu kuzuia mgomo huo kutofanikiwa dakika ya mwisho.

Wafanyakazi hao 12,000 wanagoma kupinga mipango ya British Airways ya kupunguza gharama zake. Miongoni mwa hatua zinazotazamiwa kuchukuliwa ni kupunguza idadi ya wahudumu katika ndege za safari za mbali na kutotoa nyongeza ya mishahara katika mwaka huu.

British Airways imesema itakodisha ndege kutoka mashirika mengine ya Ulaya ili kuhakikisha kuwa hadi asilimia 60 ya safari zake zitafanywa kama ilivyopangwa. Huu ni mgomo wa kwanza wa British Airways tangu miaka 13.


.

No comments:

Post a Comment