Tuesday, March 16, 2010

Tetezi:Kashfa ya ufisadi-Ununuzi wa generata katika kituo cha damu salama

Assalam Aleykum

Natanguliza shukurani zangu kwako kwa juhudi mnazozichukua katika web site yenu. kwa kweli imetuzinduwa mengi sisi wanzanzibari.Lengo na madhumuni ya barua hii , ni kukutaka na kukuarifu kuwa kuna ubadhirifu mkubwa umetokea katika benk ya damu salama hapo Sebleni.

Kwa kuwa kulikuwepo na tatizo la umeme kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu takriban, kwa kweli lilikuwa ni tatizo la kitaifa lakini hata hivyo imeonekana katika benki ya damu pamefanyika manunuzi yasikuwa ya halali ya GENERETA, KUNA GENERETA imenunuliwa isikuwa na kiwango cha ukweli ( wats) genereta hiyo imenunuliwa pasipokuwa na utaratibu mzima wa (Procuariment) yaani ugavi, inasemakana imenunuliwa kwa thamani ya milioni arbaini na sita, la kusikitisha ni kwamba genereta hiyo hadi hivi sasa tunaingia mitamboni ipo katika hali mbaya kwani inafanya kazi ya kusua sua tu.

Manunuzi hayo yamefanyika nje ya utaratibu wa kiserikali kwa kupitia wizara ya afya na utibabu.ni kweli genereta hiyo imepatiwa msamaha wa vat shilingi mioni sita. lakini kiutendaji wa kazi sio mzuri kwani la kushangaza hata warenti wa generete hiyo haupo inasemekana na imenunuliwa kwa mtu ambaye sio Suplier ANAYETAMBULIKA KISHERIA. mimi ni mzelendo mwenye nia nzuri na nchi yangu kwa kweli inauma sana kwa kuwaona viongozi wa wizara ya afya ( katibu mkuu) yupo mbele na maslahi yake tu , si kama nasema hivyi kwa chuki hapa kinachoniuma na ufisadi ulifanyika katika ununuzi wa genereta hilo.

Inatambulika kuwa wahusuika wa manunuzi ya jenereta hilo ni Katibu mkuu na Mkewe. Hata mafundi kutokla Wizara ya afya tayri walishauri Program Manager wa banki ya damu kuwa genereta hilo haina uwezo unaokubalika.Nimetuma repoti hii kwa nia nzuri tu, naomba suala hili lifanyiwe uhalali wake
Ahsante

Dondoo:

**Hii sio habari kamili, kwa vile hatujaweza kuithibitisha lakini inaashiria kuwepo kwa ufisadi wa aina fulani katika sakata hilo.

Tunaomba wazanzibari watoe ushirikiano na waandishi, mwandishi akisema jina lako litahifadhiwa manaake halitoandikwa kwenye magazeti na identity yako itahifadhiwa kwa maana ya kuwa public haitojua nani alietoa habari hizo muhimu katika jamii.

No comments:

Post a Comment