Wednesday, March 17, 2010

VITUKO VYA BONGO

Ofisa uhusiano wa Tigo bwana Jackson Mmbando (kulia) akimkabidhi jezi ya timu ya Arsenal ya Uingereza bwana Adam Kimario.
Meneja matangazo Tigo bwana Redemptus (kushoto) Masanja akimkabidhi jezi ya timu ya Chelsea ya Uingereza bwana Godfrey Rymond Katika moja ya Promotion za tigo ijuilikanayo kama Shinga kispoti
Picha inamuonesha Meya wa jiji la Dar-es-Salaam Adam Kimbisa akimkabidhi JK jezi ya Real Madrid yenye nambari 9 ambayo huwa inavaliwa na Christiano Ronaldo, Meya anamkabidhi jezi hii kutokana na mchango wa JK katika soka la Bongo.

Kwa kawaida mimi ninavyofahamu mtu hutoa kile kilicho chake, sasa je huyu Meya anagawa hii jezi kwa JK yeye ni kama nani katika timu ya Real Madrid, au watu wanaiga mambo tu bila kujua maana yake?.

Kwa nini watu hawa wote wasigawe jezi za timu zilizopo Bongo ikawa kama ni njia moja ya kulitangaza soka la bongo? Mambo mengine ni aibu tupu

Langu jicho tu.


.

No comments:

Post a Comment