Monday, March 15, 2010

SILAHA ZAWATIA MATATANI WARUNDI

Watu wawili raia wa Burundi wanatarajiwa kupandishwa mahakamani leo hii huko Sumbawanga Mkoani Rukwa baada ya kupatikana na kosa la kumiliki silaha.

Raia hao wa Burundi walikamatwa na silaha za kijeshi wakiwa na mwenyeji wao, ikiwemo bunduki aina ya (SMG) na risasi 127 katika kijiji cha Kabwe eneo la ziwa Tanganyika wilayani Nkasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa bwana Isuto Mantage, aliwataja raia hao wa Burundi ikiwa ni pamoja na Erick Niyokindi (25) na Richad Ndiyeze (33) wote ni wakaazi wa Kalitye Mtaa wa Chibitoke, Mkoani Bujumbura, Burundi.

Kamanda Mantage alisema kua watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 9 Machi mwaka huu katika nyumba moja ya kulala wageni ijuilikanayo kwa jina la Buma Guest House, wakiwa katika hatua ya kuuza bunduki aina ya SMG yenye nambari KI 342432.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa wa kipolisi watuhumiwa hao wa Burundi waliingia Nchini kinyume na sheria huku wakijifanya kama ni wauzaji wa mahindi.

Walizihifadhi silaha hio pamoja risasi katika nyumba ya mwenyeji wao ambae jina lake halikufahamika mara moja.

Polisi walifanikiwa kuwakata watu hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia mwema ya kwamba kuna watu wanajifanya wauza mahindi huku wakitafuta mnunuzi wa silaha za kijeshi.

Walipohojiwa na polisi watuhumiwa hao ambao walikua wakizungumza kiswahili kidogo, walikiri kumiliki silaha ambapo walikua wakitafuta mnunuzi.


.

No comments:

Post a Comment