Monday, March 15, 2010

MSWADA KUWAZUIA WASIOKUA WAKAAZI WA ZANZIBAR

Wasiokua wakaazi wa Zanzibar hawataruhusiwa kushiriki katika upigaji wa kura ya maoni kuamua kama Zanzibar inapaswa kua na serikali ya umoja wa Kitaifa, hii imejumuishwa katika mswada wa mapendekezo ya kura ya maoni yatakayowasilishwa kwenye baraza la wawakilishi tarehe 24 mwezi huu. ambapo Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Kiongozi Mh, Hamza Hassan Juma anatarajiwa kuwasilisha muswada.

Kwa mujibu wa kifungu cha nane katika mswada huo ni kua, watu watakao weza kupiga kura hio, ni wakaazi wa Zanzibar ambao wameorodheshwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Katika sifa ya ziada, mtu ni lazima awe anaishi katika jimbo kwa muda wa miezi 32 mfululizo.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa Zanzibar, wamesema mswada huo umebuniwa kusudi kuwabana Wazanzibari wote wanaoishi Tanganyika na wale wanaoishi nje ya nchi.

Hii ina maana pia, kwa Wazanzibari wote walikosa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kigezo cha kukosa kitambulisho cha Mzanzibri mkaazi (Zan ID) nao pia hawatashiriki katika upigaji wa kura hizo za maoni, walieleza wachunguzi.

Mswada unaweka masharti magumu kwa watu ambao wanataka kukata rufaa kutokana na matokeo ya kura hizo za maoni, na kwa yoyote ambae anataka kudadisi juu ya matokeo.

Kwa mfano, mtu ambae anataka kukata rufaa ni lazima awe anaungwa mkono na asilimia kumi ya watu waliopiga kura katika kila jimbo kwa Mikoa yote mitano.

Pia atapaswa kulipa Sh 5m/- mahakama kuu kama ni dhamana, na rufaa hio ni lazima iwasilishwe ndani ya siku 30 baada ya matokeo kutangazwa.

Kwa mujibu wa mswada huo, rufaa itasikilizwa na jopo la majaji watatu ndani ya siku 30 baada ya kuwasilishwa na uamuzi utakaotolewa na majaji hao utakua ndio wa mwisho.

Mswada umeainisha kwamba, hakuna mtu atakaeruhusiwa kukata fufaa katika mahakama ya rufaa Serikali ya Muungano.

Siku rasmin ya kupiga kura za maoni itatangazwa na Rais wa Zanzibar, kwa mujibu wa mswada huo.

Kura ya maoni juu ya uundwaji wa Serikali ya umoja wa Kitaifa, ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya Rais Amani Krume na Katibu mkuu wa chama cha CUF maalim Seif Sharif Hamad.

.

1 comment:

  1. mimi nilijua mwanzo kama haya maridhiano ni upuuzi kwani hii ni njama tu ya CCM kuzima kasi ya CUF kwa mgongo wa Uzanzibari, sasa kuna nini hapa kama si danganya toto?

    ReplyDelete