Monday, March 15, 2010

DAVID BECKHAM KUKOSA KOMBE LA DUNIA

Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza David Beckham huenda akakosa kucheza fainali zinajazo za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Afrika Kusini.

Wasi wasi huo unakuja baada ya Mchezaji huyo wa kiungo wa AC Milan kuumia mguu jana alipokua akijianda kupiga mpira wakati timu yake ilipokua ikicheza na Chievo.
Beckham katika dakika za mwazo mwanzo mwa mchezo wa jana alipasuka sehemu ya uso kwa kupigwa kiatu wakati aliporuka kupiga mpira wa kichwa.

Nae msemaji wa AC Milan amethibitisha kuvunjika kwa Beckham ambapo alisema kua Beckham alisikika akimwambia Daktari "umevunjika, umevunjika", nae kocha wa AC Milan Leonado alisema kua Beckham ana bahati mbaya, na kuumia kwake hata sisi tunajisikia vibaya.

Matumaini ya Beckam kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya nne zinaonekana kutoweka kwani huenda akakaa juu kwa muda wa miezi mitatu baada ya upasuaji, na ataondoka Italy leo hii kwa safari ya Finland kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Beckham mwenye umri wa miaka 34 sasa alihamia AC Milan kwa mkopo akitokea LA Galaxy kwa ajili ya kuinusuru nafasi yake katika kikosi cha Taifa cha Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Dunia yatakayoanza Juni 11.


.

No comments:

Post a Comment