Sunday, March 7, 2010

PAUL SCHOLES ATIMIZA MAGOLI 100 LIGI KUU YA UINGEREZA

Paul scholes jana alitimiza magoli mia moja ya Premier league baada ya kufunga goli moja, goli ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwapatia ushindi Manchester United wakati walipocheza dhidi ya Wolves, ushindi huo wa ManU jana unawawezesha kufika kileleni mwa ligi hio kwa kuwa na jumla ya alama 63 huku wakiwa wameshacheza michezo 29, ikiwa ni tofauti ya alama mbili tu dhidi ya Chelsea ambao wapo kwenye nafasi ya pili wakiwa na alama 61 na wakiwa wameshacheza mechi 28.

Hata hivyo Mashetani hao wekundu hawapumui vizuri kwa wakati huu kwa kumkosa mshambuliaji wake Wyn e Rooney ambae ni mgonjwa, hivyo kupelekea timu hio kuwa roho juu kwa vile wanatarajia kukutana na AC Milan siku ya Jumaatano kwa mechi ya Champions League.

No comments:

Post a Comment