Sunday, March 7, 2010

MTOTO MCHANGA AOKOTWA NJE YA MSIKITI HUKO UINGEREZA

Mtoto mchanga ambae aliokotwa nje ya Msikiti mmoja huko Shelton amefariki baada ya kufikishwa hospitali.
Msemaji mkuu wa polisi wa Staffordshire alisema mtoto huyo baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa University Hospital iliopo North Staffordshire ambapo alifariki masaa mawili baada ya kufika spitalini hapo.
Msemaji huyo alesema kua polisi walipigiwa simu kufika katika Msikiti huo mnamo majira ya saa 10:30am jana, baada ya mtoto huyo ambae alikua amezongwa nguo kuonekana.
Eneo ambapo tukio hilo lilitokea lilizingirwa na polisi kusudi kuwawezesha polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Afisa mpelelezi wa bwana Dave Giles alisema "tunaaka tuwasiliane na mama wa mtoto kwa haraka, ambae anahitaji matibabu.

No comments:

Post a Comment