Tuesday, March 9, 2010

NYEPESI ZA ZENJI: UMEME

Haya habari tulizonazo ni kuwa idadi kubwa ya wakaazi wa MjiMkongwe na Sehemu za Kwahani walikwisha sahau jinsi ya kuingiza salio kwa kutumia mita za TUKUZA hali iliopelekea msongamano mkubwa katika vituo vya kuuzia umeme ili wafundishwe jinsi ya uingizaji wa umeme.
Pia sehemu za Kimbesamaki, Kwamchina tatizo hilo limejitokeza huku baadhi ya watu wakiwa wameshasahau direction za switch zao baina ya switch ya ukumbini na nje, au jikoni na corridor. Na badhi ya wengine wakiwa hawajui tena jinsi ya kuwasha switch.
Baadhi ya watoto wameonekana wakipiga kelele kwa furaha na wengine wakishangaa kuona jambo jipya kwenye akili zao.
Baadhi ya wazee wanaoishi nyumba za wazee Sebleni wao wamekuwa wakiziogopa taa ambazo zilikuwa zikiwaka ndani ya vyumba vyao wakisema kuwa juwa limechomoza juu ya dari za vyumba vyao.
Mental wa kidongochekundu ulipokuwa umewashwa umeme na baadhi ya taa zikiwa on baadhi ya bulb wamezipopowa kwa mawe wakifikiri embe mbivu.
HIZO NDIO NYEPESI ZA HUKU ZENJ

No comments:

Post a Comment